Artist

Artist Image


T-LYRICS

Utangulizi: \T- LYRICS \ALFRED THADEUS LYIMO ni msanii wa muziki wa Bongo HIP HOP kutoka Afrika Mashariki nchini Tanzania. \Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama T-LYRICS.(Matamshi;; tilirikz) Alifanikiwa kujizolea umaarufu kwa mara ya kwanza mkoani Mwanza na huku akipendwa na wapenzi na mashabiki, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake \'Hustler wa Bongo\'. \T-Lyrics alikuwa gumzo na wimbo \'Hustler wa bongo\' kama single yake ya kwanza kwenye tasnia ya muziki kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake mwingine \'Passion of Luv\' kama single ya pili, ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na utaalamu aliyotumia kwenye ala ya muziki wenyewe. \Maisha Ya Awali: \T-Lyrics alizaliwa 31 Julai mwaka 1987, ni mtoto wa tano kati ya saba kwa kuzaliwa katika familia ya Mzee Thadeus Paul Lyimo. \Elimu yake ya awali ya msingi aliipata katika shule ya msingi Ngangu iliyopo Moshi vijijini ambako alihitimu mwaka 2001, na kujiunga na elimu ya sekondari ya Lombeta iliyopoko Moshi vijijini na kuhitimu elimu yake ya sekondari . Mwaka 2015 alijiunga elimu ya chuo kwa kipindi cha miaka mitatu na kuhitimu na diploma ya “Architecture Designing”. \Muziki: \T-Lyrics alianza kujihusisha na masuala ya muziki mwaka 2003, na kilicho sababisha ajiingize katika fani hiyo ni Baba yake Mzazi kwa kipindi akiwa mdogo baba yake alikuwa akimletea kanda za tape za wasanii wa zamani zikiweno shabarans,luck dube na wengine wengi… \Kadri miaka ilivyozidi kusonga na kumaliza shule ya msingi alijiunga na elimu ya secondary na kuanza kujihusisha na muziki mwaka 2002.Lakini hakuanza kuimba moja kwa moja, bali alikuwa akifuatilia tu jinsi gani muziki unavyokua, na mwaka 2003 ndipo nilipojiingiza zaidi kwa kuanza kuimba katika sherehe mbalimbali za makempu.na shuleni. Pia alikuwa akikariri mistari ya wasanii na kutafuta biti za nyimbo hizo alizokariri na kuanza kuimba. \"Alianzisha kikundi cha kuimba katika shule ya sekondari hapo kiitwacho ‘ADIZOME’ hii ilikuwa na muunganiko wa wanafunzi wane ambao ni Alfred,Dickson,Zeno na Michael.Alikuwa pia ni mtunzi mzuri wa mashairi na walimu na wanafunzi walimtumia sana kutunga mashairi ya mahafali ya kila mwaka kwa kipindi chake chote akiwa secondary. \Alipohitimu elimu yake ya secondari alijiunga na elimu ya chuo ngazi ya diploma na kupata fani ya usanifu majengo. Kipindi akiwa chuoni alijiunga na kwaya ya hapo na alianzisha tena kikundi cha kuimba baada ya kukutana na mwanachuo mwenzake aitwae William Mfilima a.k.a Real Nate. Waliunda kikundi kiitwacho ‘ZOMINATE EMPIRE’ \Baada ya kumaliza chuo kila mmoja aliendelea na maisha yake wakati huo T-Lyrics akawa ameenda mwanza kutafuta riziki. \Ndipo akaanza kujihusisha rasmi na maswala ya muziki ‘2008, ila mwaka 2009 alifanikiwa kukutana na mmoja wa produza maarufu nchini ‘MARIJAN RAJAB’na kuweza kurekodi ngoma yake ya kwanza iitwayo ‘Hustler wa Bongo” katika studio za ‘REFLEX PRODUCTION’. \Baada ya kuonekana uwezo wake mkubwa sana uongozi wa studio ulimpa ofa ya kurekodi wimbo uitwao ‘Number One’ aliowashirikisha ‘L TO DA P’ na ‘MARY G’ \Kipindi cha mwaka huo wa ‘2009’niliachia ngoma ya kwanza iitwayo ‘Hustler wa Bongo ’ ikapendwa sana na wasikilizaji mpaka kupelekea kujulikana sana mtaani na kupata show mbalimbali jijini Mwanza. Alifanikiwa kufanya video yake ya kwanza chini ya ‘REFLEX VISION’ chini ya producer ‘Pul Lmeck’. \Mwaka ‘2010’ alirekodi wimbo wangu mwingine uitwao ‘Passion of Luv’ aliomshirikisha mwanadada ‘MAGGY’ kwenye studio za ‘MO-RECORDS’ zilizopo Ilemela Mwanza. Ilifaanyiwa video na ‘HANS NEW PAGE’ hatimaye ikafanya vizuri kwenye media za televisheni na kufikia hadi mkali wa wiki ‘STAR TV’. \Wimbo wa ‘Passion of Luv’uliendelea kumpa umaarufu zaidi na kuonesha uwezo wake wakubadilisha staili kutoka muziki wa HARD HIP-HOP aliyo anzia kwenda kwenye COMMERCIAL HIP HOP. \T- LYRICS ©Mandusu Enterprises Ltd 2015 \T- LYRICS \Ufupisho: \JINA LA KUZALIWA ALFRED THADEUS LYIMO \JINA LA KISANII T- LYRICS \AMEZALIWA 31 JULAI 1987 (Umri 27 YRS) \AINA YA MZIKI BONGO HIP HOP \KAZI YAKE MUIMBAJI \ALA SAUTI \MIAKA YA KAZI 2002 - Present \STUDIO REFLEX PRODUCTION,MO-RECORD, CLASSIC SOUND, DM RECORDS \LABEL NORTH MUSIC SIDE (NMS), \MANDUSU ENTERPRISES \AMEWASHIRIKISHA Q THE DON, MARY G, MAGGY, NURUELLI, OX OKELEKY, YSTAR, AYLER, TIDDY \ ...
Read More...Welcome to Mkito.com's new look. Let us show you around...
This is a song. You can see the image, song name, artists and you can interact with it by previewing, downloading or sharing it with your friends.
To listen to a 30 second preview of any song, you can click the preview button under the name of the song.
To share a song with friends, you can click this share button and choose from the share options
If you want to go through all the artists we have here on Mkito, you can click here to browse through our artists lists.
To look through our music by genre, you can click here and select a genre of your choice.
To download a song,you can click on the download button of the song you like. You must be logged in to download a song.
If you have an account with Mkito, you can sign in by clicking this link, which will open a popup window.
From here, you can select your login method.
To use your email address or phone number to log in, click this button.
Enter your details and click the button to log in.
Or create a new account here
If you don't have an account with Mkito, you can sign up by clicking this link, which will open a popup window.
From here, you can select your signup method.
To use your email address or phone number, click this button,which will take you to the registration form.
To register as an artist, click here.
Or you can use your Facebook, Twitter or Google Accounts to sign in.