Artist

Artist Image


Gadiely Kayanda

Naitwa Gadiely Kayanda. Toka utoto wangu nilipenda sana kuimba na mara kwa mara ungenikuta naimba pekee yangu chumbani, chooni, barabarani, na popote pale ambapo nilipata nafasi ya kukaa pekee yangu. Mara baada ya vipindi vya jioni nilipenda kwenda kuangalia kwaya za kanisani kwetu zinavyoimba, hata ikafikia hatua nikatengeneza gitaa kwa kuchonga upande wa kuni na kuuwekea nyuzi za kushonea viatu. Lakini mama yangu alinikataza na kutishia kunipiga nalo, niliamua kuliacha, mpaka kipindi hicho nilikuwa bado sijatambua kipawa nilichonacho cha kuimba na kutunga nyimbo. 2005- Nilipokuwa kidato cha kwanza ndipo nilipoanza kutunga nyimbo zaidi ya ishirini na zote zilikuwa za kidunia na hasa bongo fleva . Wimbo mmoja ambao niriurekodi kwenye redio kaseti ya mama yangu ulikuwa unaitwa “Maisha ya shule” mpaka leo upo. 2007- Nilihama shule baada maombi ya mda mrefu kutoka Nyarubanda sekondari kigoma vijijini kwenda kentoni sekondari ya dar es salaam. Niliamua kuzichoma nyimbo zote za bongofleva ingawa nilikuwa bado sijaokoka kwa sababu niliona kama sitazitumia tena maana nilikuwa naona msimu mpya mbele yangu kwa namna ambayo kwa jinsi ya mwilini nisingeweza kueleza. 2008 -April siku ya jumatatu ya pasaka nilipokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu nikiwa sebuleni naangalia video ya kusurubishwa kwa Yesu msalabani. 2010 -Nikiwa katika maombi ya UKWATA Darpwani muhimbili kwenye ofsi za Tafes nilisikia ngoma(drums), gitaa, vinanda vikipigwa moyoni wangu. Nilishangaa kwa sababu ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na kitu kama hicho, mwanzoni nilifikiri ni watu wanaotangaza matangazo barabarani, lakini nikagundua siyo. Nikasikia sauti inaimba wimbo moyoni mwangu nikaamua kuifuatilia kwani ulikuwa ni wimbo mpya sijawahi usikia sehemu yoyote. Siku ile ndipo nilipopata wimbo wangu wa kwanza wa kikiristo unaoitwa “Tunakushukuru” kwenye albamu hii haumo, utakuwemo kwenye albamu itakayofuata. 2011- Nilipomaliza kidato cha sita niliamua kujiunga na kikundi cha kusifu na kuabudu cha kanisa la KKKT usharika wa Mabibo farasi. Ilikuwa kama nimetibua kisima cha maji yaliyotuama au nimechokoza nyuki, nilianza kuota usiku nikiwa naimba au naongoza kuimba mbele ya watu wengi na nyimbo nilizokuwa naimba zilikuwa ni mpya, nahubiri, naombea watu mpaka mapepo yanatoka. 2012-2014- Nikawa muimbaji wa kwaya na kikundi cha kusifu na kuabudu katika umoja wa wanafunzi wa kikristo Tanzania chuo cha mipango Dodoma. Hapo ndipo baadhi ya nyimbo zangu zilianza kupewa nafasi na kuimbwa na waimbaji wenzangu. Nilishangaa kuona kila wimbo niliokuwa nautambulisha kwa watu walikuwa wanaupenda, walinitia moyo na nikazidi kutunga nyimbo nyingi zaidi. 2013- Mwezi September niliamua kuingia studio kurekodi nyimbo hizi ili kuzitunza kwa ajili ya vizazi vya leo na kesho. Nimekamilisha albamu hii mwaka 2014 october kutokana na uhaba wa fedha. ...
Read More...Welcome to Mkito.com's new look. Let us show you around...
This is a song. You can see the image, song name, artists and you can interact with it by previewing, downloading or sharing it with your friends.
To listen to a 30 second preview of any song, you can click the preview button under the name of the song.
To share a song with friends, you can click this share button and choose from the share options
If you want to go through all the artists we have here on Mkito, you can click here to browse through our artists lists.
To look through our music by genre, you can click here and select a genre of your choice.
To download a song,you can click on the download button of the song you like. You must be logged in to download a song.
If you have an account with Mkito, you can sign in by clicking this link, which will open a popup window.
From here, you can select your login method.
To use your email address or phone number to log in, click this button.
Enter your details and click the button to log in.
Or create a new account here
If you don't have an account with Mkito, you can sign up by clicking this link, which will open a popup window.
From here, you can select your signup method.
To use your email address or phone number, click this button,which will take you to the registration form.
To register as an artist, click here.
Or you can use your Facebook, Twitter or Google Accounts to sign in.